Kadhi Mkuu afafanua utata ulioibuka kuhusu siku kamili ya Udd Ul Adha

564 views · Published 22 August 2018 · 2:19 · Indexed 27 September 2026

Channel: KTN News Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Kadhi mkuu Ahmed Muhdhar amefafanua mdahalo kuhusu siku kuu ya Idd Ul Adha ambapo utata uliibuka kuhusu siku kamili ambapo waislamu wanatakiwa kuadhimisha siku hiyo.

Baadhi ya waislamu humu nchini waliadhimisha siku hiyo hapo jana huku wengine wakiiadhimisha hivi leo. Kulingana na kadhi mkuu Wakenya wanapaswa kufuata dalili za humu nchini na si mataifa mengine. 

Aidha baadhi ya viongozi akiwemo seneta wa Mombasa Mohammed Faki na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff wamepinga vikali kuundwa kwa mufti ili kushughulikia tofauti zinazojitokeza katika sherehe za jamii ya Waislamu. Wamedai kuwa tofauti za kuuona mwezi zimekuwepo tangu jadi na azimio la kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale kamwe halitafua dafu.


SUBSCRIBE to our YouTube channel for more great videos: https://www.youtube.com/
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KTNNews  

Like us on Facebook: https://www.facebook.com/KTNNewsKenya 

For more great content go to http://www.standardmedia.co.ke/ktnnews and download our apps:
http://std.co.ke/apps/#android 




KTN News is a leading 24-hour TV channel in Eastern Africa with its headquarters located along Mombasa Road, at Standard Group Centre. This is the most authoritative news channel in Kenya and beyond.

More from this channel