Mtoto mmoja wa Kikei aliyepotea amepatikana
1,771 views · Published 11 October 2018 · 1:03 · Indexed 1 October 2026
Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics
Mmoja wa watoto wawili walioripotiwa kutoweka eneo la Thika kaunti ya Kiambu amepatikana hii leo baada ya NTV kuangazia visa hivyo viwili jioni. Mercy Wagio Karanya alipatikana akirandaranda ovyo ovyo , akiwa ameonekana kuchanganyikiwa. Kwa sasa Mercy mwenye umri wa miaka kumi na miwili yuko katika kituo cha polisi cha Thika alikopelekewa baada ya kupatikana na wasamaria wema. Awali mama yake alikuwa amepiga ripoti katika kituo cha polisi cha Makongeni, Thika, bintiye alikuwa amepotea mtaani Makongeni phase 10. Hata hivyo mtoto mwingine wa kiume Alvin Ngari Kwera mwenye umri wa miaka minne ambaye vilevile amedaiwa kutekwa nyara katika eneo lilo hilo angali kupatikana. Inadaiwa Alvin alitekwa nyara akiwa na mwanafunzi mwingine wakiwa kanisani siku ya Jumapili . Kijana aliyekuwa ametekwa naye aliachiliwa baada ya siku moja. OCPD wa Thika Paul Kiriki alisema maafisa wa polisi wanachunguza watu kadhaa katika kijiji hicho ili kuwakamata watekaji nyara hao.
More from this channel
-
4:13
IEBC begins clearing candidates for MP countrywide
-
1:06
Sports journalist apologises for attack on Damian Marley
-
2:17
Kenya Red Cross Society says the drought is still far from over
-
2:37
Retired Nyeri archbishop accused of speaking for the government during Madaraka Day prayer
-
4:34
Iyanya performs some of his greatest hits on #theTrend
-
4:42
T412 perform 'Flee' on #TheTrend
-
0:23
T412's Milome explains the reason behind Nasa hao
-
8:19
Gilad and Superband reveal the inspiration behind Nairobi Yangu