Waziri Matiang’i aonya wanaokiuka sheria za barabarani

256 views · Published 25 December 2018 · 1:57 · Indexed 18 October 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Wahudumu wa magari ya uchukuzi ya umma, abiria na madereva wa magari ya kibinafsi wanaovunja sheria barabarani watafikishwa mahakamani mara moja na kukabiliwa vikali na sheria. Akisema hayo, waziri wa usalama, Fred Matiang’i, ameshikilia kuwa maafisa wa polisi wameachia likizo zao ili wawe kazini kuhakikisha wakenya wako salama majumbani na barabarani na hawatafanya mzaha na yeyote anayejaribu kuhatarisha maisha ya wakenya barabarani.

More from this channel