Ronaldinho azuru Kisumu; Gaucho atoa mafunzo ya soka katika kaunti hiyo
4,324 views · Published 10 November 2018 · 0:36 · Indexed 12 October 2026
Channel: NTV Kenya · 2018 · Sports
Aliyekuwa kiungo mahiri wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldo de Assis Moreira maarufu Ronaldinho Gaucho amezuru kaunti ya Kisumu na kuendesha kliniki ya soka huko. Ronaldinho Gaucho mwenye umri wa miaka 38 yuko kenya kwa hisani ya kampuni ya Betika na kwa ushirikiano na Extreme Sports ambayo ni mwandalizi wa ligi ya Super 8. Hapo kesho nyota huyo aliyewahi kuichezea Barcelona ya uhispania, Paris Saint-Germain ya ufaransa na AC Milan ya Italia atashuhudia mechi ya ligi ya mabingwa ya supa 8 kati ya mabingwa jericho na TUK uwanjani Camp Toyoyo. Gaucho anakumbukwa kwa mbwembwe zake anapokuwa na mpira uwanjani mbali na kushinda kombe la dunia mwaka wa 2002 akiwa na Brazil.
More from this channel
-
4:13
IEBC begins clearing candidates for MP countrywide
-
1:06
Sports journalist apologises for attack on Damian Marley
-
2:17
Kenya Red Cross Society says the drought is still far from over
-
2:37
Retired Nyeri archbishop accused of speaking for the government during Madaraka Day prayer
-
3:53
Tanzanian farmers, like Kenyans, eagerly awaiting the use of GMOs - Food Friday
-
4:34
Iyanya performs some of his greatest hits on #theTrend
-
4:42
T412 perform 'Flee' on #TheTrend
-
0:23
T412's Milome explains the reason behind Nasa hao