Ndoa iliyotibuka Nakuru yaibua hisia tofauti kuhusu uchunguzi wa HIV

1,483 views · Published 6 November 2018 · 2:33 · Indexed 27 September 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Jesse Karanja mhubiri aliyedaiwa kusitisha ndoa Nakuru anasemekana kuwataka wanandoa hao wawili kufanya uchunguzi wa kiafya. Kulingana na familia za wanandoa hao, walihitajika kufanya uchunguzi wa virusi vya HIV na kuwasilisha matokeo kwa mhubiri huyo. Licha ya kuwa matokeo ya uchunguzi huo haujulikani na sababu halisi ya kusitishwa kwa ndoa hiyo kutokuwa wazi, kulingana na jopo linaloangazia masuala ya HIV na AIDS, sio sawa kwa mtu kulazimishwa kufanya uchunguzi wa HIV na zaidi ya hapo kuwataka kuweka wazi hali yao ya HIV.

More from this channel