Watahiniwa waliokosa adabu; Makachero wafika katika shule ya upili ya Ambira

3,153 views · Published 23 November 2018 · 1:02 · Indexed 30 October 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Makachero kutoka idara ya upelelezi wa  jinai DCI hii leo wamefika katika shule ya upili ya Ambira huko Nyanza kuchunguza matamshi ya matusi ambayo yalirekodiwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na wanafunzi chuoni humo. Katika video hiyo ya sekunde thelathini, wavulana hao walionekana wakichoma vitabu, kuashiria kuwa wamekamilisha masomo ya sekondari, huku wakiwatusi mawaziri  wa usalama wa ndani  Fred matiangi na Amina Mohammed wa elimu.  Wanafunzi waliokuwa kwenye kikao hicho wametambuliwa kama Opiyo Brantley Owino , Hongo Steven ,  Barry Oduor Odhiambo ,  Odhiambo Ralph Lauren ,  Omondi Joshua Otieno ,   Edwin Omondi, Clinton Oduor Onyango  na Lavin Jude Ombago.

More from this channel