Raga ya Safari 7s: Timu za Kenya zimeingia robo fainali

191 views · Published 10 November 2018 · 0:43 · Indexed 28 September 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · Sports

Watch on YouTube

Timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande Shujaa imeingia robo fainali ya kuwania ubingwa wa raga ya safari sevens  katika uwanja wa  RFUEA,  Nairobi.

Shujaa imefuzu pamoja na Kenya Morans, Samurai na Uhispania. Shujaa iliadhibu Apache alama 42 kwa 0 na kisha ikaishinda  Mwamba alama 53 kwa 0. Morans iliinyuka ureno alama 12 kwa 5 na kushinda alama 19 kwa 12 dhidi ya Uganda. Samurai iliifunga Uganda II alama 50 kwa 17 na kisha kuilaza Red Wailers alama 27 kwa 5 nayo Uhispania iliifunga  Red Wailers alama 19 kwa 14 kabla ya kuifunga  Uganda II alama 24 kwa 19.

More from this channel