Walimu 15 wazuiwa rumande Kisii kuhusiana na wizi wa KCSE

1,494 views · Published 6 November 2018 · 2:28 · Indexed 7 October 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Walimu kumi na watano wameshtakiwa katika mahakama ya Ogembo katika kaunti ya Kisii kwa madai ya kuhusika na udanganyifu wa mtihani. Mahakama imeamua wasalie rumande uchunguzi ukiendelea. Kwingineko aliyekuwa gavana wa Nairobi, Evans Kidero, ameitaka mahakama kusimamisha uchunguzi kuhusu ufisadi alipokuwa gavana unaoendeshwa na tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini, EACC. Kwa mujibu wa Kidero, mali yake nyingi inayochunguzwa na EACC aliipata kabla ya kuwa gavana wa Nairobi.

More from this channel