Matatu zarejea katikati mwa jiji la Nairobi

1,254 views · Published 4 December 2018 · 2:33 · Indexed 7 October 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Hali ya kawaida imerejea katika barabara za Nairobi hii leo baada ya kusitishwa kwa marufuku ya magari ya usafiri wa umma kuingia katikati mwa jiji. Mahakama kuu imetoa amri kusitisha marufuku hiyo baada ya mfanyibiashara, Paul Kobia, kuifahamisha mahakama kuwa Gavana Mike Mbuvi Sonko anaweza kutangaza tena marufuku hiyo baada ya kuisitisha alfajiri.

More from this channel