Polisi wamzuilia mama anayedaiwa kuua na kujeruhi watoto wake

838 views · Published 13 October 2018 · 1:53 · Indexed 23 September 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Polisi wanamzuilia mama anayedaiwa kumuua mwanawe kwa kumchinja kabla ya kujaribu kumuua mwanawe wa pili eneo la Baragoi kaunti ya Samburu. Kwa mujibu wa polisi mama huyo alimkata kwa kisu shingoni mwanawe wa miaka 2 na kumuua huku jaribio lake la kumuua bintiye wa miaka 7 likitibuka pale binti huyo alipofanikiwa kutoroka japo akiwa na majeraha mabaya ya kisu shingoni. Uchunguzi unaendelea kubaini nia ya mama huyo.

More from this channel