Kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa gavana Samboja yatupiliwa mbali

487 views · Published 15 January 2018 · 1:03 · Indexed 21 September 2026

Channel: NTV Kenya · 2018 · News & Politics

Watch on YouTube

Mahakama kuu mjini Voi imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na wapiga kura wawili kupinga kuchaguliwa kwa gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja.

Akitoa uamuzi huo jaji Eric Ogolla anasema mahakama hiyo haina uwezo wa kubaini kuhusu tuhuma dhidi ya Samboja kughushi vyeti vyake vya masomo na badala yake tume ya kukabili ufisadi EACC ndio yenye jukumu hilo.

 Jaji Ogolla anasema walalamishi katika kesi hiyo hawakushawishi mahakama hiyo kwamba samboja alishiriki katika udanganyifu wa kura katika uchaguzi wa agosti nane.

Wakili wa Samboja Edwin Ayiro amesema amefurahishwa na uamuzi huo huku akisema sasa mteja wake atakuwa huru kufanya majukumu yake akiendelea na kesi moja ambayo iko mahakama ya milimani.Walalamishi hao wawili ,Arstrong Kiwoi na Thomas Njumwa wameagizwa kulipa shilingi nusu milioni.

Gavana Samboja alielekea katika kanisa la ACK lilioko mjini Voi kutoa shukrani na  Kusherekea ushindi  pamoja na wafuasi wake .

More from this channel